Safari yetu ya kutamani

Fuatilia hadithi yetu na kujitolea kwa ubora kwa mistari michache tu

Hadithi yetu

Malengo yetu kwa sasa!

Kila mtu aweze kusaidia kuhakikisha kuwa tunafikia Malengo ya Ulimwengu.

01
Kupambana na magonjwa ya kuambukiza


Kukomesha milipuko ya UKIMWI, kifua kikuu, malaria na magonjwa mengine yaliyosahaulika na kupambana na homa ya ini, magonjwa yatokanayo na maji na magonjwa mengine ya kuambukiza.

02
Kupunguzavifo kutokana na magonjwa yasioambukiza na kukuza Afya ya Akili

Kupunguza vifo vya mapema kutokana na magonjwa yasiyoambukiza kupitia ufahamu na upatikanaji wa kinga na matibabu na kukuza afya ya akili na ustawi.

03
Kuzuia na kutibu matumizi mabaya ya Dawa

Kuimarisha uzuiaji na matibabu ya matumizi mabaya ya dawa za kulevya, na matumizi mabaya ya pombe.

04
Upatikanaji wa huduma za Afya ya uzazi​

Tunahakikisha upatikanaji wa matibabu ya magonjwa ya ngono na huduma za afya ya uzazi kwa wote, ikijumuisha elimu ya uzazi wa mpango.

05
Kupunguza magonjwa na vifo kutokana na kemikali hatari na uchafuzi

Kupynguza kwa kiasi kikubwa idadi ya vifo na magonjwa kutokana na kemikali hatari na uchafuzi wa hewa, maji na udongo.

06
Kudhibiti matumizi ya tumbaku

Kuimarisha utekelezaji wa Mkataba wa Mfumo wa Shirika la Afya Duniani kuhusu Udhibiti wa Tumbaku katika nchi zote, kadri inavyofaa.

07
Kuunga mkono tafiti, maendeleo na upatikanaji wa chanjo na dawa

Kusaidia utafiti na uundaji wa chanjo na dawa za magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza ambayo kimsingi yanaathiri nchi zinazoendelea, kutoa ufikiaji wa dawa na chanjo muhimu kwa bei nafuu.

08
Kuboresha utambuzi wa ishara hatari za kiafya

Kuimarisha uwezo wa kutambua mapema ishara hatari za kiafya mapema, kupunguza hatari na udhibiti wa hatari za afya za kitaifa na kimataifa.

FOR NHIF

Call 199​ Free
www.nhif.or.tz