Kwanini wanawake wengi huchelewa kugundulika na kuanza matibabu ya saratani ya matiti?

Saratani ya matiti, au Kansa ya matiti, ndiyo saratani inayoongoza kwa vifo vya wanawake ulimwenguni. Wengi wanakumbwa na kuchelewa kugundulika na kuanza matibabu sahihi, hivyo kuongezeka kwa idadi ya vifo vinavyohusiana na ugonjwa huu.

Zaidi ya asilimia 70% ya wanawake huanza matibabu ya saratani ya matiti katika hospitali za rufaa wakiwa hatua mbaya. Wengi wanakuja wakiwa na titi lililoharibika, kidonda kwenye titi, harufu mbaya, kushindwa kupumua kutokana na saratani kusambaa kwenye mapafu, na kuvimba mkono wote upande wa titi lililoathirika. Hii ni hatua ya nne ya ugonjwa huu.

breastmx

Wanawake wengi huchelewa kugundulika na kuanza matibabu ya saratani ya matiti kwa sababu zifuatazo:

Wengi hujiusisha na matibabu ya tiba mbadala, kwa takriban (48%) ya wagonjwa waliokuwa wanapatiwa matibabu katika Hospitali za Rufaa ikiwemo Muhimbili na Ocean Road waliousishwa kwenye tafiti iliyokwishafanyika walikuwa wakijihusisha kwa muda mrefu zaidi na

Japo kuna tafiti zilifanywa juu ya mti na matunda ya mstafeli juu ya kupambana na saratani, ikaoneshwa mmea huu unauwezo wa kupambana na saratani hasa kuzuia saratani (yaani kuzuia kuenea kwa seli za saratani) lakini hakukua na uthibitisho wa kutibu ugonjwa wa saratani.

tiba

Kunaambao hutumia tiba mbadala hata baada ya kuthibitika Hospitalini kuwa na saratani ya matiti, hii inatokana na imani za kidini, desturi za watu wetu, tamaduni na uelewa wao wa saratani kama “shambulio la kiroho”. Hii hupunguza kwa kiasi kikubwa uanzishwaji wa dawa maarufu kama kemo kwa wagonjwa na hata uwezekano wa kufanyiwa upasuaji kuondoa uvimbe katika hatua za awali za ugonjwa.

Kuna wengine kutokana Gharama za  matibabu ikiwa Pamoja na vipimo, gharama za upasuaji au dawa za kutibu saratani huwafanya kuchelea kuanza matibabu na kujikita kwenye tiba mbadala.

Juhudi za Serikali katika kuhakikisha huduma za bima ya afya kwa wote na kuweka huduma hizo kwenye mfumo wa bima na juhudi za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na wahisani katika kuhudumia wagonjwa wa saratani zinaweza kupunguza mzigo wa kifedha kwa wagonjwa.

wengi hudhani akigundulika kuwa anasaratani ya matiti basi atafanyiwa upasuaji wa kuondolewa titi yaani mastectomy. Kuna imani potofu ya watu kwamba upasuaji wa kuondolewa titi mara nyingi husababisha kifo baada ya upasuaji. Tafiti zinaonyesha kuwa 10% ya wagonjwa huchelewa kuanza matibabu kwa sababu ya kuogopa upasuaji wa kuondolewa titi. Kwa kuwa upasuaji wa kuondolewa titi ni sehemu muhimu ya udhibiti wa saratani ya matiti, hasa katika  hatua mbaya ya ugonjwa. kugundulika mapema kwa wagonjwa wapya wa saratani kunaweza kupunguza hofu hii kwani kwenye hatua za awali za ugonjwa hakuitajiki upasuaji wa kuondolewa titi. Bali upo upasuaji wa kuondoa uvimbe tu bila kuathiri titi yaani mgonjwa anabaki na matiti yake yote.

surgery

Hii ni sababu ya nne inayosababisha wanawake wengi kuchelewa kuanzanza matibabu ya saratani baada ya kuthibitika kuwa anasaratani. Kemo kama ilivyozoeleka ni dawa zinzotumiwa kutibu saratani kwa kuua seli za saratani, kuzuia saratani isisambae au kupunguza uvimbe wa saratani, inakuwa katika hali ya kimiminika au kidonge na kutolewa kwa kunjywa au sindano (yaani dripu). Wagonjwa wengine pia walihusisha hofu ya kemo dhidi ya athari zake kuhisiwa “zinasababisha kifo”. Mtoa huduma ana jukumu kubwa la kutekeleza katika kuhakikisha kuwa wagonjwa wanashauriwa vizuri. Ingawa inaweza kuwa haifai kutafuna maneno katika kuelezea athari za dawa, inaweza kuwahakikishia wagonjwa kuwa kemo zina athari kama ilivyo dawa zingine tu, na athari zake ni za muda na mara nyingi zinaweza kubadilishwa.

Pia, kuna wakati mgonjwa kuchelewa matibabu kutokana muda uliotumika kwa mtoa huduma wa kwanza (toka mgonjwa anakutana na Daktari wa kwanza) kwenye Hospitali ndogo au vituo vya Afya hadi pale anapopatiwa Rufaa. Kimsingi mwanamke mwenye viashilia vya saratani ya titi anatakiwa mapema kuanza kufanyiwa vipimo vya saratani katika Hospitali za Rufaa ilikubaini kama uvimbe huo ni saratani au la. Sasa unakuta mgonjwa anapewa rufaa lakini kutokana na sababu mbalimbali za mgonjwa mwenyewe mfano sababu za kifedha au Hofu ya matibabu zinaweza pelekea kuchelewa matibabu toka mgonjwa apate Rufaa hadi kuanza kwa matibabu.

ambulance
examofbreast

Inatakiwa angalau ndani ya miezi 10 baada ya kua na viashilia vya saratani hadi itakapothibitika kua ni saratani ya matiti mgonjwa awe ameanza matibabu, japo kuanza kwa matibabu ndani ya siku 45 za kwanza baada ya kugunduliwa kwa saratani ya matiti  huongeza Umri wa kuishi na kumfanya aweze kuendelea na kazi zake hata baada ya matibabu, ilhali kucheleweshwa kunapunguza umri wa kuishi na wengi kushindwa kuendelea kufaya kazi zao za kawaida hata baada ya matibabu kutokana na athari ya kusambaa kwa saratani kwenye mifupa na mapafu kumfanya awe mchovu muda wote, wengine kushindwa kutembea na kuvimba sehemu za mwili kama vile tumbo, mkono uliokaribu na titi lililoathirika. Hivyo basi kuchelewa kunaweza kusababisha matokeo mabaya zaidi.

  1. Kwenye familia kuna aliyepata ugonjwa huu, hivyo amejifunza kupitia changamoto zilizomkuta mwezake.
  2. wanafunzi wa vyuoni. na hii ni kutokana na matumizi ya mitandao huwafanya wanapoona utofauti katika miili yao huwapelekea kuperuzi unakuta tayari ana elimu kiasi kuhusu saratani hii hata kabla ya kuonana na mtaalamu wa afya.
  3. wahudumu wa afya. kumbuka saratani inaweza mpata mtu yeyote na wakati wowote hivyo kwa wahudumu wa afya ambao hua na dalili za saratani hii huwai matibabu sababu wana elimu juu ya ugonjwa huu.
Elimu ya afya ni muhimu sana katika kukabiliana na saratani, kwani inasaidia kuongeza uelewa wa jamii kuhusu magonjwa hayo.
0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments